Kumekucha ni mchezo wa radio utakaozinduliwa July 25, ukitazama mchango wa wanawake na vijana katika kutokomeza tatizo la uhaba wa chakula nchini Tanzania.
Mchezo wa Kumekucha ni wa kila wiki ambapo unaangazia maisha, vikwazo, na fursa za wakulima wa Tanzania. Mchezo utaanza kurushwa hewani July 25, nchi nzima. Mchezo utaruka hewani kila wiki mara moja kupitia Radio Free Africa (Taifa), Abood FM (Morogoro), Ebony FM (Iringa) and Bomba FM (Mbeya).
Wasanii wakubwa wa Bongo Movie kama vile JB, wachekeshaji Mau na Monica Sizya, na pia wanamuziki maarufu ‘JFK’ John Kitime na Mataluma, wamo katika mchezo huu uliochezewa katika maeneo ya mashambani nchini Tanzania.
Mchezo wa Kumekucha ika korido ya SAGCOT. Mchezo huu utaangazia zaidi juhudi za wanawake na vijana katika kilimo.
Sekta ya kilimo ni moja ya sekta muhimu katika uchumi wa Tanzania, inachangia 25% ya pato la taifa na 25% ya mazao yanaoyouzwa nje ya nchi. Kilimo kinaajiri Watanzania kwa asilimia 75, wengi wao wakiwa ni wanawake na vijana.
Wakati wanawake wakiwa ndio sehemu kubwa ya uzalishaji wa chakula hapa Tanzania, wengi wao hawana sauti katika maamuuzi yanayofanyika katika ngazi ya familia, hasa kwenye mgawanyo na matumizi ya mazao ya jasho lao.
Sheria na tamaduni zilizopo zinakwaza juhudi za wanawake kupata fursa za kiuchumi kwa sababu hawana haki ya kumiliki ardhi, au vifaa bora vya kilimo, vyanzo endelevu vya maji, ukosefu wa mikopo ambayo wanahitaji ili kufanikisha juhudi zao. Vikwazo hivi vinawazuia wanawake kujikwamua na umasikini, kupatia lishe bora familia zao, na pia kufikia malengo yao ya kuwa wakulima wa kisasa.
Vivyohivyo, vijana nao wanawakilisha theluthi tatu ya waajiriwa wote katika sekta ya kilimo, lakini mara nyingi ajira zao ni za muda mfupi au vibarua, wanaotegemea kudra za majira na mikataba isiyo na manufaa yeyote kwao.
Mchezo wa Kumechucha umeandaliwa na Africa Lead, kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI), na kufadhiliwa na U.S. Agency for International Development (USAID). Watayarishaji wa Kumekucha, MFDI, waliwahi pia kutayarisha mchezo mwingine wa radio wa Wahapahapa na pia mchezo wa runinga wa SiriyaMtungi. Mchezo huu umefadhiliwa na watu kutoka Marekani (USAID) na nia yake hasa ni kupunguza uhaba wa vyakula vyenye virutubisho hapa Tanzania. Tunafanya hivi kwa kuongeza fursa za kiuchumi – hasa kwa wanawake na vijana – katika sekta ya kilimo
Kumekucha umetayarishwa chini ya ushauri wa Tanzania Food and Nutrition Center (TFNC), Tanzania Horticultural Association (TAHA), ACDI VOCA – NAFAKA, Land O Lakes, RUDI, MWANZO BORA, The Rice Council of Tanzania, Technoserve, ANSAF (Non State Action Forum) na AMSHA (Youth in Agribusiness Forum).
Mbeya (88.8 MHZ), Dodoma (89.0 MHZ), Dar es Salaam (89.3 MHZ), Iringa/Njombe (89.9 MHZ), Morogoro (93.8 MHZ)
Tuesdays: 10:30 – 11 am
Saturdays: 10:30 – 11 am
Iringa (87.8), Njombe (88.2), Mbeya (94.7), Dar es Salaam (106.9)
Saturdays: 6 – 6:30 pm
Sundays: 6 – 6:30 pm
Mbeya (104.0 FM)
Mondays: 6:30 – 7 pm
Saturdays: 8 – 8:30 am
Dodoma (106.9 FM), Morogoro (89.9 FM), Dar es Salaam (101.7 FM)
Tuesdays: 6:30 – 7 pm
Wednesdays: 6:30 – 7 pm
Saturdays: 9:30 – 10 am
EPISODE 01
|
EPISODE 02
|
EPISODE 03
|
EPISODE 04
|
EPISODE 05
|
EPISODE 06
|
EPISODE 07
|
EPISODE 08
|
EPISODE 09
|
EPISODE 10
|
EPISODE 11
|
EPISODE 12
|
EPISODE 13
|
EPISODE 14
|
EPISODE 15
|
EPISODE 16
|
EPISODE 17
|
EPISODE 18
|
EPISODE 19
|
EPISODE 20
|
EPISODE 21
|
EPISODE 22
|
EPISODE 23
|
EPISODE 24
|
EPISODE 25
|
EPISODE 26
|
EPISODE 27
|
EPISODE 28
|
EPISODE 29
|
EPISODE 30
|
EPISODE 31
|
EPISODE 32
|
EPISODE 33
|
EPISODE 34
|
EPISODE 35
|
EPISODE 36
|
EPISODE 37
|
EPISODE 38
|
EPISODE 39
|
EPISODE 40
|
EPISODE 41
|
EPISODE 42
|
EPISODE 43
|
EPISODE 44
|
EPISODE 45
|
EPISODE 46
|
EPISODE 47
|
EPISODE 48
|
EPISODE 49
|
EPISODE 50
|
EPISODE 51
|
EPISODE 52
|
Mama ni mkulima. Baba ni mdudu mharibifu.
Mwanamke wa kijijini, mfuata desturi, siku zote amekuwa akihatarisha mwili na nafsi yake, bila thawabu au ahsante, kwa kulima shamba la mume wake, kulisha na kuhudumia familia yake. Anapambana na hali mbaya za hewa, wadudu waharibifu, na umaskini. Lakini pale Manyusi anapotumia vibaya mavuno yake ya thamani, na anapopanga mbinu ya kumuoza binti yao, Fatuma analazimika kupambana na mume wake.
Filamu ya Kumekucha – Tunu (Zawadi) ni hadithi ya Mashoto, ambaye anafanya kazi kama kondakta wa daladala mjini. Maisha ya Mashoto mjini ni ya upambanaji. Dar es salaam in maisha ya anasa, na Mashoto anapenda hivyo. Hana muda wa kufikiri juu ya watu na maisha aliyoyaacha kijijini, mpaka anapopata taarifa ya msiba wa mama yake.
Anaporudi nyumbani kwa ajili ya msiba, huzuni ya kumpoteza mama yake inamfanya achanganyikiwe. Anaamini ardhi imelaaniwa na hataki kusikia lolote kuhusu hiyo. Baba yake, Sanga anapoteza matumaini juu yake. Baada ya muda kidogo, anajikuta anafanya kazi na dalali mwenye dhuluma, Kidevu. Ni mapambano magumu kwa Mashoto, wakati anajitahidi kutafuta dhumuni ndani ya kijiji.
Lakini bado, mama yake amemuachia zawadi. Sauti yake, na uwepo wake usioonekana, sauti inayomuambia kwa upole afungue macho na kuzibua masikio yake, ili aweze kujifunza somo juu ya uoto wa asili wa dunia na mizizi itoayo rutuba kutoka kwenye hiyo.
Baada ya kufukuzwa nyumbani na baba yake kwa kutumia pesa kidogo alizoziacha mama yake, Mashoto lazima ajifunze kuishi kwa kutegemea ardhi. Lazima ajifunze jinsi ya kukabiliana na maadui wa zamani na kutafuta marafiki wapya. Lazima ajifunze kupambana na kupenda. Lakini jambo la muhimu zaidi, Mashoto lazima atambue kile anachokipigania.