The Writers

Uncategorized Comments (0)

char-writers

‘Maisha ya wakulima yanafanyiza igizo zuri kabisa la redioni’

Kwa watunzi watatu wa igizo la redioni, Kumekucha, imekuwa ni safari ya ugunduzi katika sehemu zenye uzalishaji mwingi wa kilimo, Tanzania.

Mhariri wa Filamu Cece Mlay na watunzi wake Amina Lukanza na Kheri Mkhali walianza safari hii katika warsha ya wiki mbili jijini Dar es Salaam, Machi 2016, ambapo wataalamu wa sekta husika walifunguka kuhusu nafasi ya mwanamke na kijana katika kilimo.

Wataalamu kutoka kwenye taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali walichangia mawazo juu ya kilimo cha Tanzania, yaliyozingatia taarifa za ukweli na zilizofanyiwa utafiti, na huku wakionyesha video juu ya kilimo cha mboga-mboga, uvumbuzi katika sekta, huduma za sera na uenezi, masoko, bei, mazao na usafirishaji, na vile-vile ushuhuda (usio rasmi) wa watu binafsi ambao ulitoa taarifa nyingi juu ya hali ya maisha vijijini. Warsha haikuishia tu kwenye kuonyesha uwezo mkubwa wa kiuchumi katika kilimo cha Tanzania, bali pia hazina kubwa ya maigizo yenye kuleta shauku/kuvutia katika jamii za wakulima.

“Maisha ya wakulima yana simulizi nyingi, na zinafaa kabisa kwa igizo la redioni”, anasema Mtunzi Mkuu – Cece Mlay.

Watunzi walienda kwenye sehemu zenye uzalishaji mwingi wa kilimo ili kuchunguza kwanini baadhi ya sehemu zenye utajiri mkubwa nchini bado zina umaskini na utapiamlo. Wakiwa na ujuzi wa mambo ya ndani ya nchi, wakazindua “ulimwengu wa kufikirika ambao huenda usijulikane kwa mara ya kwanza, lakini ukaendana na uhalisia” kwa hadhira yetu vijijini.

Walitengeneza mji wa kufikirika kama kijiji chochote kilichopo kwenye ukanda wenye rutuba wa SAGCOT, uitwao Lunyanja. Walikipa kijiji ghala lake, soko dogo, barabara iliyopinda-pinda katika vilima na mto wenye kona nyingi, mto Makeke. Walielezea kwa kina maisha ya kila siku na mazingira ya wahusika wakuu. Walifumbua pepo za kawaida na uelekeo ambao mvua hutokea. Walitengeneza jamii yenye wahusika waliotiwa chumvi waishio katika changamoto, furaha na hali ya kukosa matumaini/kutoridhika na maisha ya kijijini.

Kisha, watunzi walizipenda simulizi za maisha ya wahusika wao.

“Hili ni igizo kuhusu watu ambao wanahangaika na nafsi zao wenyewe, ardhi na tamaa/shauku ya kuwa juu,” anasema Cece Mlay.

“Tunafurahia kutoa simulizi hizi,” anasema Amina Lukanza. “Tunatumai kwamba ubora wa matokeo ya mwisho utaakisi hili.”

» Uncategorized » The Writers
On July 1, 2016
By

Comments are closed.

« »